• Breaking News

  May 12, 2016

  Uchambuzi huru: Jakaya Kikwete anafuata nyayo za Rais Vladimir Putin?

  Rais wa sasa wa Urusi ndugu Vladimir Putin alihakikisha anatimiza ndoto yake ya kudumu ndani ya ikulu ya Moscow kwani aliamini kuwa bila yeye Urusi itayumba!

  Ili kutokuvunja katiba ya Urusi, kijanjajanja alimpachika mtu wake Dmitry Medvedev kuwa rais kwa kipindi kimoja ili atakapogombea tena asiambiwe kuwa amevunja katiba ya Urusi kwa kugombea awamu tatu mfululizo! Ili kuzuia hilo, alijipa uwaziri mkuu kisha akamuweka mtu awe rais wa Urusi ambaye alikuwa huyo Dmitry Medvedev. Hata hivyo, kipindi cha utawala wa Dimitry, Vladimir Putin ndiye aliyekuwa akiiwakilisha ikulu ya Moscow kwenye vikao mbalimbali na hasa ndiye alikuwa msemaji mkuu wa dola la Urusi kimataifa! Baada ya utawala wa Dmitry Medvedev, bwana Putin alirejea katika usukani wake wa kuitawala tena ikulu ya Moscow kwa awamu nyingine mbili kama rais! Hakuulizwa kwani alikidhi vigezo vyote vya kugombea achilia mbali kuwahi kuitawala Urusi kwa miaka kumi hapo kitambo kidogo!

  Tanzania tunaye rais mstaafu wa awamu ya nne ndugu Jakaya Kikwete! Mbali na kuwa na rais wa nchi John Magufuli, Kikwete ndiye amekuwa kioo cha nchi kimataifa!

  Kikwete ameshafanya vikao vitatu ndani ya nchi kuisemea Tanzania kimataifa, vivyo hivyo
  vikao vitatu nje ya nchi ambapo viwili barani Afrika na kimoja ulaya!

  Mbali na ukweli kuwa Kikwete hatarajii tena kurejea katika ikulu ya Dar es Salaam kama Putin wa Russia, lakini anatoa tafsiri ya walakini kwa rais Magufuli. Kiukweli inaonekana kuwa rais Magufuli ama ameonyesha wazi kuwa na uwezo mdogo kuiwakilisha Tanzania kimataifa au ana matatizo ya kusafiri umbali mrefu kama inavyosemwasemwa! Ila kwa kiongozi mkuu wa nchi, hii inatoa tafsiri ambayo siyo nzuri na inafifisha nguvu ya utawala wa Magufuli!

  By G Sam

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku