• Breaking News

  May 6, 2016

  Uliipata MSG ya sheria mpya DSM? Kabla ya kupewa chumba Guest mnapigwa picha? Meya kaongea

  Ijumaa ya May 6 2016 kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hususani Whatsapp najua utakuwa ulipokea ujumbe ambao ulikuwa unaripotiwa kuwa umetoka kwa meya  wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita, ujumbe uliokuwa umeenea ulikuwa unahusisha kuwa meya wa Dar es Salaam Isaya Mwita ametangaza sheria mpya.

  Meya Isaya Mwita ameeleza kuwa ujumbe unaoenea kuwa ametangaza sheria mpya Dar es Salaam sio wa kweli na umetungwa na watu ambao wanapanga kumchafulia jina lake.


  Ujumbe wa uongo ambao ulisambazwa leo May 6 2016 na kudaiwa umetoka kwa meya wa Dar es Salaam

  “Sio kweli kuwa kuna sehemu nimetoa statement ya namna hiyo ila huyo atakayekuwa ameandika atakuwa na lengo tofauti, kwa hiyo naomba wananchi wapuuze hiyo statement ambayo imekuwa ikisambaa, bahati mbaya sikuwahi kupata mtu akiuliza maoni yoyote kuhusiana na tukio hilo la Kimara ila kwa upande wangu sijatoa tamko lolote”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku