• Breaking News

  May 11, 2016

  ''Unanawishwa Mikono Chakula Hupewi''-Nassari


  Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari amesema kitendo cha serikali kupeleka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuchimba mashimo ya kuweka nguzo za umeme na kubaki hivyo bila ya nguzo na umeme kufikishwa ni kuwanawisha na kuwanyima chakula.

  Mbunge Nassari ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma katika mkutano unaoendea wakati wa maswali na majibu katika wizara ya Nishati na Madini.

  Mheshimiwa Mwenyekiti Kuna juhudi zimefanyika huko nyuma za kupeleka umeme vijijini lakini sasa hivi jimboni kwangu kuna vijiji ambavyo REA walichimba mashimo na kuyaacha wazi wakati wananchi walifyeka mazao yao serikali haioni kwamba kitendo hiki ni sawa na kuwanawisha mikono na kuwanyima chakula, ni lini serikali itapeleka nguzo na kuwafungia wananchi hawa umeme?

  Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani amesema vijiji vyote nchini ambavyo vipo katika awamu ya tatu ya mradi wa REA vitapatiwa umeme baaada ya wabunge kupitisha bajeti ya wizara hiyo na fedha kutoka kwenda kuendeleza miradi hiyo.

  Dkt. Kalemani amewaondoa wasiwasi wabunge wanaopitiwa na miradi hiyo kwamba watakwenda kushughulikia kero ya umeme kuanzia mwezi wa saba 2016.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku