• Breaking News

  May 12, 2016

  Ushauri wa Rais Magufuli kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni


  May 12 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais huyo iliyofanyika katika uwanja wa Kololo Jijini Kampala.

  Baada ya Rais Magufuli kutoa pongezi kwa Rais wa Uganda, viongozi hao wamezungumzia mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta la kutoka Hoima (Ziwa Albert) nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo pamoja na kuishukuru Uganda kwa uamuzi wake wa kuamua bomba hilo lipitie Tanzania.

  Rais Magufuli amemshauri Rais Museveni kufupisha muda wa ujenzi wa mradi huo, kwa kutumia mbinu inayojumuisha usanifu na ujenzi (Design and Construct method) na kutumia wakandarasi wengi watakaogawanywa katika vipande tofauti badala ya kutumia mkandarasi mmoja.
  ”Nashauri tutumie mbinu ya usanifu na ujenzi pamoja, hii ni njia ya haraka zaidi, na pia tugawe vipande vya ujenzi kwa njia yote ya bomba la mafuta yenye urefu wa kilometa 1,410 tunaweza kuwa na Wakandarasi watano mpaka sita ambao watatumia njia hiyo mpya ya usanifu na ujenzi.
  ”Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza muda utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, inaweza hata kuchukua mwaka mmoja tu” :-Rais Magufuli.

  Rais Magufuli amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo faida za mradi huo wa mafuta zitaanza kupatikana mapema badala ya kusubiri miaka miwili au mitatu ijayo na kwamba hiyo itakuwa inaendana na kauli mbiu yake ya “Hapa Kazi Tu”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku