• Breaking News

  May 17, 2016

  Utamchukia Zitto Kabwe Lakini Akiongea Anamwaga Sumu Tupu

  Donald Trump ni mwanasiasa anayefanana sana na dunia ya sasa ya vitu vinavyopatikana haraka haraka. Trump ni mwanasiasa asiyetabirika, muda wowote ule anaharibu hali ya hewa kwa uropokaji wake. Ni mjanja mwenye kujua kuwa watu wa kizazi cha kisasa hawataki sana mambo ya takwimu, hawataki sana kusikia sera mbalimbali na jinsi zitakavyoweza kutekelezeka.

  Hillary Clinton ni tofauti kabisa, yeye ni kama alivyo mumewe (Bill Clinton), yupo tayari kumwaga sera kwa kuongea kwa muda mrefu bila ya kujali kama wanaomsikiliza wameanza kusinzia au kupiga miayo.

  Zitto Kabwe ni aina ya Hillary na Bill Clinton. Haendani sana na kizazi chake, ambacho siku zote kinataka mambo ya haraka haraka, kinataka kusikia jinsi gani leo inavyoweza kuwa bora zaidi.

  Unaweza kumchukia Zitto Kabwe labda kwa sababu ya ile intellectual Superiority Complex lakini jamaa kila akifungua mdomo bungeni anamwaga sumu nzito. Tena anazidi kukomaa katika ule utulivu wa kuchukua muda anaopewa kwa ajili ya kujenga hoja.

  Katika dunia ambayo Hillary na Bill Clinton wanaingia kwenye miaka ya sabini, wanaibuka wanasiasa vijana wenye kusimamia katika mantiki (substance) badala ya mihemko ya muda mfupi.

  Zitto Kabwe asichoke kusoma vitabu vingi kutoka kwa watu walioelimika, tabia hiyo inamsaidia katika kujenga hoja nzito.

  Donald Trump anawafaa hawa waliozaliwa miaka ya karibuni wenye kupenda vituko na vichekesho lakini mantiki ikiwa zero.

  Keep it up Zitto Kabwe.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku