• Breaking News

  May 26, 2016

  VIDEO: Uchambuzi wa Edo Kumwembe kuhusu Van Gaal kufukuzwa Man United

  Bado wapenzi na mashabiki wa Man United wanasubiri ile siku atakayotangazwa rasmi kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Louis van Gaal ndani ya klabu ya Man United, Ayo TV ilipata nafasi ya kumtafuta mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe ili atoe tathmini yake.

  “Ni kweli Van Gaal alikuwa anahitaji muda zaidi wa kujenga timu, kwani Van Gaal ana CV kubwa katika vilabu alivyopita ila anahitaji misimu mitatu minne ili aweze kupata mafanikio, halafu Van Gaal sio kocha wa kufundisha mastaa huwa anawapa nafasi wachezaji wachanga”

  “Kwa Man United kwa sasa wanahitaji kujenga image ya klabu yao ambayo itaiwezesha kulinda brand yao ya biashara, hivyo Mourinho ni mtu sahihi kuitoa shimoni klabu hiyo, kwani Mourinho ni kocha mwenye rekodi ya kutwaa mataji katika msimu wake wa kwanza”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku