Watu wa usalama katika bunge la Afrika Kusini wamewaondoa wabunge wa Upinzani wa chama cha Economic Freedom Fighter baada ya kujaribu kuzuia Rais Jacob Zuma asihutubie.

EFF wamesema Rais Zuma hasitahili kuhutubia bunge kutokana na maamuzi ya mahakama dhidi yake hivi karibuni, baada ya kiongozi wa EFF,  Malema Julius kutolewa bungeni  aliwaambia waandishi wa habari: ’Hatuwezi kuongozwa na mtu ambaye alishindwa kutekeleza, kutetea na kuilinda katiba’


Post a Comment

 
Top