• Breaking News

  May 3, 2016

  Vyombo vya Habari vilifanya vizuri Uchaguzi Mkuu

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamend Chande Othman amesema kwamba vyombo vya habari nchini vimefanya kazi kubwa sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Jaji Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wadau wa vyombo vya habari ambao wamekusanyika jijini Mwanza katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ambapo kauli mbiu mwaka huu inasema kupata habari ni haki yako idai.
  Jaji mkuu amesisitiza kuwa vyombo vya habari viliweza kufanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi na pia kutoa habari kuhusiana na mwenendo mzima wa uchaguzi jambo ambalo lilifanya wananchi kuweza kushiriki kikamilifu.

  Aidha ameongeza kuwa kukua kwa teknolojia ya 'internet' nchini kumechangia wasomaji wa magazeti kupungua kutokana na wananchi kupata taarifa kupitia mitandao ya kijamii ila bado changamoto hiyo siyo kubwa sana.

  Mei 03 ya kila mwaka dunia huadhimisha siku ya vyombo vya habari ambapo wadau wa vyombo vya habari hushiriki katika makongamano maalum, katika kujadili mambo yanayokwamisha uhuru wa vyombo vya habari pamoja na namna ya kusonga mbele kiutendaji.

  Maadhimisho kwa upande wa Tanzania yanafikia kilele leo ambapo wadau wa habari zadi ya 250 wameungana mkoani Mwanza ambapo Waziri wa Habari Nape Nnauye na Mwenyekiti wa Vyombo vya Habari Dkt. Regnald Mengi ni miongoni mwa wageni walioalikwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku