• Breaking News

  May 12, 2016

  Wafanyabiashara Coco Beach Waomba Wapatiwe Eneo

  Wafanyabiashara katika ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam wameiomba serikali kuwapa umiliki wa muda wa eneo hilo ili waweze kutumia kama dhamana ya kuombea mikopo kutoka taasisi za fedha.

  Wamesema kuwa iwapo watapata mikopo hiyo, itawasaidia katika kuboresha eneo hilo na kuwa kivutio maalumu cha utalii na biashara nchini kutokana na kuwa na ufukwe mzuri wa mchanga.

  Wakizungumza kupitia Kiongozi wao Bw. Bernard Mwinuka; wafanyabiashara hao wamesema kwa muda mrefu wameshindwa kuendeleza ufukwe huo na biashara zao kutostawi kama ilivyotarajiwa kutokana na kutokuwa na mtaji wa kutosha wa kuendeleza biashara hizo.

  Mwinuka amefafanua kuwa licha ya Ufukwe wa Coco Beach kubeba taswira halisi ya mandhari ya jiji la Dar es Salaam; hali yake hivi sasa haivutii idadi kubwa ya watalii kutembelea eneo hilo kama ilivyo kwa fukwe za nchi nyingine zinazopokea watalii wengi kama vile Angola, Brazil, Chile na visiwa vya Caribbean.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku