• Breaking News

  May 17, 2016

  Waitara Ahoji Vituo Vidogo vya Polisi Kufungwa Saa Kumi na Mbili Jioni

  Mbunge wa Ukonga jijini Dar es Salaam Bw. Mwikwabe Mwita Waitara, amehoji sababu za jeshi la polisi kufunga vituo vidogo vya polisi saa kumi na mbili jioni, wakati ambao uhalifu unaombatana na uporaji unapoanza kushamiri katika maeneo mengi ya kijamii.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Pugu Kajiungeni, Bw. Waitara amesema kitendo cha jeshi la polisi kimesababisha kushamiri kwa matukio hayo na kuleta hofu kwa wananchi, hivyo ameahidi kufuatilia suala hilo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Charles Kitwanga.

  Katika mkutano huo, Mbunge huyo aliwaeleza wananchi hatua anazochukua kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilala kutanzua changamoto mbalimbali katika sekta za elimu hususan upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa pamoja na kuimarisha huduma kwenye sekta za afya na maji.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku