• Breaking News

  May 16, 2016

  Wananchi Wafunga Barabara ya Mwanza -Musoma na Wawe...Kisa Hichi Hapa


  Wananchi na Wakazi wa Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, mapema leo wamefunga barabara ya Mwanza-Musoma katika eneo la Kisesa na hivyo kusababisha abiria wanaoingia Jijini Mwanza kutoka Mikoani kukwama barabarani kwa zaidi ya saa moja.

  Wamechukua maamuzi hayo baada ya dereva wa daladala moja kumgonga mtoto katika eneo hilo. Taarifa za awali zinaeleza kwamba mtoto huyo amefariki papo hapo.

  Baada ya hatua hiyo, jeshi la polisi, kikosi cha kuzuia ghasia limefika eneo la tukio na kuwasihi wananchi kufungua barabara hiyo ili kutowakwamisha abiria kuendelea na safari zao huku hatua zaidi za kisheria zikifuata dhidi ya dereva aliesababisha ajali hiyo kwani baada ya ajali alijisalimisha polisi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku