• Breaking News

  May 19, 2016

  Wananchi Zanzibar wamekuwa na wasiwasi na uwezo wa serikali yao wa kukusanya kodi.

  Pamoja na wafanyakazi wengi kufurahia kiwango kipya cha mshahara   cha shilingi laki tatu bado wananchi wengi wamekuwa na wasiwasi na uwezo wa serikali wa kukusanya kodi kikamilifu.

  Wakizumgumza na ITV kwa nyakati tofauti kuhusu bajeti ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyowasilishwa jumatano na waziri wa fedha Dr Khalid Mohamed baadhi ya wakazi wamesema ongezeko la mshahara  ni jambo zuri lakini wasiwasi mkubwa wa serikali kushindwa kukusanya kodi inavyotakiwa, nao baadhi ya wafanyakzi wameonekana kushangazwa na mshahara huo mpya kuanza mwakani April na sio mwaka huu.

  Serikali ya Zanzibar imetangaza bajeti yake ya shilingi bilioni 841.5 huku ikitangaza kutokuwepo kodi mpya, ongezeko la bei la bidhaa na pia kutangaza kuweka kiwango kipya cha mshara wa kima cha chini cha laki tatu na kupunguza kodi ya mshahara kutoka asilimia 13 hadi tisa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku