Wanawake katika jimbo la Ndeiya nchini Kenya walifahamisha kuwa waume zao wanashindwa kuwapa ujauzito kutokana na mwenendo wa unywaji wa pombe haramu ambazo zinaathiri nguvu za kiume.

Katika maandamano ya amani yaliofanyika katika kituo cha biashara cha Thigio, wanawake walioandamana Akhamisi walifahamisha kukerwa na wanaume wanaojihusisha na ulevi kupita kiasi.
Nancy Wangare alifahamisha kuwa katika kijiji 
hicho wanawake wachache walioolewa wamevumilia kwa kiasi kikubwa kutokana na upungufu wa nguvu za kiume kwa waume zao kutokana na pombe wanazokunywa.
Mmoja miongoni mwa wanawake walikuwa wakiandamana alifahamisha kuwa iwapo tabia hiyo ya ulevi haitorekebishwa basi itawalazimu kutoka nje ya ndoa zao na bila wao kujua lolote na kuwahudumia watoto wasiokuwa wao
Post a Comment

 
Top