• Breaking News

  May 6, 2016

  Watu Sita Wasakwa na Polisi Kwa Mauaji

  Watu sita wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wanatafutwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumuuwa dereva Joseph Abubakari(32) mkazi wa Mkundi manispaa ya Morogoro kwa kumpiga kwa risasi sehemu ya kichwani.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Aprili 30 mwaka huu majira ya saa 2.30 usiku huko eneo la Kilongo kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.
  Matei amesema majambazi hao walifanya mauaji hayo kwa kutumia silaha aina ya Mak lV iliyokuwa na risasi ambazo idadi yake haikufahamika pia walimshambulia Derigo Joseph(34) mfanyabiashara na mkazi wa Mkundi.

  Aidha amesema watu hao baada ya kutekeleza uhalifu huo walipora simu mbalimbali za mkononi zipatazo sita na fedha taslimu shilingi 130,000 kisha kutokomea kusikojulikana.

  Aidha kufuatia tukio hali hiyo jeshi la polisi mkaoni hapa likafanya msako maalumu katika maeneo mbalimbali kwa nia ya kusaka wahalifu kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo lilifanikiwa kukamata silaha mbili aina ya shortgun na risasi tano katika matukio mawili tofauti.

  Kamanda huyo amesema silaha hizo zilikamatwa maeneo ya Kingolwira Mei 2 mwaka huu majira ya saa 3 majira ya asubuhi baada ya kumpekuwa Boniface William(50) mkulima na mkazi wa Kingolwira huku silaha hiyo ikiwa imetengenezwa kienyeji na kukatwa mtutu na kuwekwa katika mfuko wa nailoni kisha kufukiwa Ardhini katika shamba la mtuhumiwa.

  Katika tukio lingine Joseph Mayanda((38) mkazi wa Kihonda anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya shortgun na risasi 1 iliyotengenezwa kienyeji.

  Tukio hilo lilitokea Nei 5 mwaka huu majira ya saa nane mchana huko kata ya Kihonda manispaa ya Morogoro ambapo silaha hiyo ilipatikana baada ya kupekuliwa katika nyumba yake na kwamba mtuhumiwaanaendelea kufanyiwa mahojiano na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku