• Breaking News

  May 16, 2016

  Waziri Mkuu Majaliwa Atoa Sababu Kuu Kwanini Bunge Lisirushwe Laivu


  Akizungumza na Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini London, Uingereza hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliulizwa suala la Bunge kutooneshwa ‘LIVE’ tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ameeleza kuwa hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwawezesha watu kufanya kazi kama ambavyo kaulimbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu inavyosema.......

  “Bunge la Tanzania lilikuwa ni bunge pekee katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani ambalo lilikuwa likirushwa LIVE kuanzia asubuhi hadi usiku. Ina maana katika kipindi cha Bunge la Bajeti, ambalo linaendeshwa kila siku kwa miezi mitatu, Watanzania nao wangekuwa LIVE kwa miezi mitatu,” alisema.

  “Tulilazimika kujifunza kutoka kwenye mabunge mengine. Hivi hapa Uingereza mnaangalia Bunge live kila siku?” alihoji Waziri Mkuu na kujibiwa kuwa linarushwa LIVE kwa kipindi kisichozidi dakika 15 wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu pekee.

  Akitoa ufafanuzi, aliwaeleza kwamba Bunge la Tanzania linarusha ‘LIVE’ kila siku asubuhi wakati wa maswali ya kawaida na Alhamisi asubuhi wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu lakini mijadala yote hurekodiwa na kuhaririwa na kisha kurushwa kuanzia saa 8-9 mchana na saa 3-4 usiku kwa siku husika.

  Kwa Watanzania wanaopenda kufanya kazi na wanapenda kufuatilia mambo ya Bungeni, walikuwa hawaoni ‘LIVE Coverage’ kwa sababu walikuwa kazini lakini sasa hivi wanaweza kufuatilia masuala ya bunge kwani muda wa jioni uliopangwa mtu anakuwa ametoka kazini na anaweza kuangalia televisheni akiwa nyumbani baada ya kutoka kazini.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku