• Breaking News

  May 17, 2016

  Zitto Kabwe amtaka Nape aziagize redio na TV za TZ zicheze asilimia 80 nyimbo za nyumbani

  May 13 2016 ilikuwa ni siku ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017 .

  Hotuba hiyo iliyosomwa na Waziri, Nape Nnauye ambapo kiwango kilichoombwa kilikuwa ni shilingi 20,326,176,000.

  Wabunge mbalimbali walichangia bajeti hiyo huku Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe yeye alikuwa na haya ya kusema katika uchangiaji wake wa Wizara hiyo kuhusu muziki wa nyumbani:

  “Leo hii ukifungua Redio au TV za hapa nyumbani zote asilimia nyingi utakuta wanapiga nyimbo za nje tu. Leo hii ukienda nchi za watu kuna limit mfano ukienda Lagos,Nigeria ukisikia nyimbo ya msanii wa huku kwetu basi ujue lazima atakuwa amefanya na msanii wao yaani wana promote wasanii wao, sasa sisi sijui ni ulimbukeni wa ukoloni wa miaka hamsini bado haujatutoka. Nape hili lipo kwako kama unataka kuwatetea wasanii hili wala halihiitaji kubadilisha sheria na kanuni za kontenti zipo chini ya waziri. Toa kanuni TCRA wazibariki kuwa asilimia 80 ya nyimbo zitakazopigwa kwenye redio na TV zetu ziwe za wasanii wetu wa Tanzania basi,” alisema Zitto.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku