Kambi rasmi ya upinzani bungeni sasa inauona utawala wa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda kuwa ulikuwa na hekima ya uongozi kwa kumaliza tofauti na wabunge bila kushindana.

“Makinda alikuwa akiona mmeenda kinyume tu anawaandikia kimemo, mbunge mmoja mmoja akiwataka mkutane ofisini kwake na kumaliza. Hakukuwa na mwanya wa kushindana tofauti na Dk Tulia,” amesema Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, David Silinde.

 Amesema kukosekana kwa Spika Job Ndugai ambaye amekuwa bungeni kwa muda mrefu kumesababisha mgawanyiko kati ya wabunge wa upinzani na wa chama tawala.Post a Comment

 
Top