Jun 28, 2016

Bungeni: Watakaowapa mimba wanafunzi miaka 30 Jela

Bunge limepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Namba Mbili wa 2016, huku baadhi ya wabunge wakitaka adhabu ya kifungo cha miaka 30 kwa atakayempa mimba mwanafunzi iongezewe viboko na malipo ya fidia ya malezi ya mtoto.

Katika marekebisho ya Sheria ya Elimu, Sura ya 353, Serikali inapendekeza kuanzisha zuio la kuoa au kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari na atakayetiwa hatiani, atafungwa miaka 30 gerezani.

Wabunge waliochangia muswada huo walieleza kuwa maboresho hayo yatasaidia kupunguza vitendo vya wanafunzi kupachikwa mimba na wanaume, maarufu kwa jina la mafataki, ambao huishia kulipa faini ya Sh500,000 au kifungo kidogo cha miaka mitatu kwa kosa la pili, adhabu waliyodai ni ndogo.

Hata hivyo, uliibuka wasiwasi kuwa huenda baadhi ya watu wakafungwa kwa kubambikiziwa ujauzito, hivyo kupendekeza katika ushahidi wa suala hilo, vipimo vya vinasaba (DNA) vitumike kabla na baada ya watoto kuzaliwa ili kuthibitisha iwapo aliyefungwa ni baba wa mtoto.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR