• Breaking News

  Jun 10, 2016

  Diamond Ashindwa Kulipia Plate Number Yenye Jina Lake

  Kama mtakumbuka, siku chache zilizopita nilitoa angalizo kuwa matumizi mabaya ya fedha ya kijana wetu Diamond yanaweza kupelekea nyota huyu kufilisika na kujikuta anaungana na wasanii wengine waliowahi kung'aa lakini wameshafulia.

  Kana kwamba Mungu alikuwa pamoja nami, leo utabiri wangu unaanza kutimia.

  Akiongea na kipindi cha Amplifaya cha CLOUDS FM na kutoa maoni yake juu ya uamuzi wa serikali kupandisha ada ya kulipia number plate kwa watu wanaoweka majina yao kutoka shs milioni 5 hadi 10, mwanamuziki huyo amesema hana tena mpango wa kuweka jina kwenye gari lake na sasa atarudia utaratibu wa zamani wa kuweka namba kama watu wengine wafanyavyo.

  "Unajua ule ulikuwa ni ujana tu, na mtu ukiwa kijana unataka kujaribu kila kitu. Ila kwa sasa nimeshakua hivyo sitoweka tena jina langu". Alisikika akijishaua nyota huyo wa WCB akijaribu kujikakamua ili kuonyesha ni kukua ndiyo kumemfanya abadili maamuzi lakini WENYE AKILI tumemshtukia.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku