• Breaking News

  Jun 28, 2016

  Jukwaa huru la wazalendo latoa neno kuhusu teuzi za Wakuu wa Wilaya wapya

  JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  VIONGOZI WATEULE TUKACHAPE KAZI KWELI KWELI​

  Ndugu waandishi wa habari salaam!
  Poleni na majukumu ya kila siku ya ujenzi wa Taifa.
  Leo Jukwaa Huru La Wazalendo Tanzania, tumewaiteni hapa kueleza na kupongeza jitihada za mh John Joseph Pombe Magufuli rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea wananchi maendeleo yao wenyewe.

  Ndugu wana habari, JuhWaTa linatumia fursa hii kwanza kabisa, kumpongeza mh rais kwa teuzi za wakuu wa wilaya alizofanya hivi karibuni. Mh rais amezidi kudhihirisha kuwa yeye ni kiongozi anayeishi na kusimamia kile anachoahidi kwa vitendo, mh rais alisema nanukuu "... _Nimeona vijana ndio wachapakazi, wasiopenda rushwa na Wazalendo, hivyo nitaendelea kuwaamini ndani ya serikali yangu kwa kuwateua kunisaidia kazi mbalimbali_ ..." mwisho wa kunukuu na hili amelitimiza na kulithibitisha katika teuzi hizi za wakuu wa wilaya ambapo kwa zaidi ya 70% ya wateuliwa wote ni vijana. Sote tunajua vijana wana ari, utayari na shauku ya kuongoza kwa sifa za kiuongozi ambazo ni Uadilifu, Ubunifu, Uwajibikaji na Uzalendo. Hongera sana mh rais.

  Ndugu wana habari, Jukwaa limefurahishwa kwa kitendo cha mh rais JP Magufuli kwa kuzidi kujipambanua zaidi na zaidi kuwa yeye ni rais wa Watanzania wote pasipo kujali itikadi zao husasan za kisiasa. Teuzi hizi zimesadifu taswira nzima ya mh rais kwani amezingatia zaidi Uadilifu, Uwajibikaji, Uzalendo na uwezo wa kiongozi husika katika kuunganisha wananchi ili kufikia maendeleo yao wenyewe na Taifa kwa ujumla kuelekea kuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati. Tunampongeza sana.

  Ndugu wana habari, Jukwaa pia linawapongeza wateule wote kwa kupewa heshima kuu na imani ya pekee kutoka kwa mh rais pia tunatoa Rai kwa Wateule wote ya kuendelea kujitathmini na kujiuliza mara mbili mbili ni vigezo gani mh rais ametumia kuwaamini wao na sio wale? Ni imani ipi rais amewapa wao na sio hawa wengine? Nawashauri wakafuate hatua na kuendelea kumjengea mh rais imani juu ya vijana vile walivyofanya vijana wenzao waliotangulia katika nafasi mbalimbali za Ukuu wa Mikoa, Ukatibu mkuu, Uwaziri, unaibu waziri, Ukuu wa Wilaya nk iliyopelekea kufungua milango kwa vijana wengi zaidi. Kachapeni kazi njema mzidi kufungua milango mingi zaidi kwa vijana wengine.
  Jukwaa limejiridhisha kuwa mh rais ni kiongozi asiyependa kutenda kwa mazoea, Mazoea ni kujisahau. Tukachape kazi kweli kweli ya kumsadia mh rais katika adhma yake ya dhati ya kuwatumikia Watanzania wote bila kujali rangi zao, dini zao, sehemu zao na vyama vyao. Maendeleo ni ya Watanzania wote na Taifa kwa ujumla.

  Kwa kuhitimisha Jukwaa linatoa Rai kwa Watanzania wote, viongozi wote wa dini na kisiasa tuendelee kumuunga mkono mh rais katika harakati zake za kutuletea maendeleo Watanzania wote.
  Pia Tunawatakia ndugu zetu Waislam wote mfungo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Na kila la kheri timu ya Yanga African wawe na mchezo wa ushindi dhidi ya timu ya TP Mazembe ya DR Congo.
  Ahsanteni sana.

  *Imetolewa* _28/06/2016_ DSM.
  Mtela Mwampamba.
  Katibu Jukwaa Huru La Wazalendo Tz. 0755178928

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku