• Breaking News

  Jun 14, 2016

  Mkapa aunguruma: Tanzania inahitaji Mijadala ya wazi tena Makini, agusia Katiba iliyokwama

  Anasema kiongozi lazima asikilize. Hii nchi tutaiendeleza sisi wenyewe. Tuache kugombana bila Uchambuzi wa Kina. Ametolea mfano Mkwamo wa katiba, kasema ilitakiwa tuchambue na kutafakari Nini kiliikwamisha na nini kifanyike sio kulaumu tu.

  Kasema ukiwa unaongea sana inabidi tutafakari jinsi ya kukudhibiti sababu saa nyingine mtu akiongea sana anakutoa kwenye njia na Malengo.

  Asema nchi yetu Tanzania ndiyo yenye magazeti mengi, ingekuwa ndo kipimo basi sisi tumeendelea kweli kweli.

  Mkapa amesema yeye ndie aliemuita Agha Khan aje aanzishe magazeti mengine hapa ndiyo yakaja mengine ya Mwananchi na the Citizen.

  ''Kwa mfano Prof Shivji amezungumzia kuhusu uhusiano wa kibiashara kati ya powerful block na nchi za Afrika, je ni uhusiano gani wa kibiashara utakaokuwepo kati ya wenye nguvu na wasio na nguvu?'' Alisema Mkapa

  Amesema tunapenda kuzungumzia watu kuliko sera. Fuatilia michango ya wabunge Vijana Bungeni ambao wengine wanatoka hapa chuo kikuu, wana hoja gani? Wanazungumza nini? Video:

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku