Jun 3, 2016

Polisi Waanza Kutekeleza Adhabu "kali" kwa Madereva Wanaovamia Barabara za Mwendo Kasi

Jeshi la Polisi limeanza kutekeleza mtindo mpya wa kuwaadhibu madereva wote wanaotumia barabara ya mabasi ya mwendo kasi na kuvunja sheria za Barabarani.
Mtindo huo wa adhabu unajumuisha kumkamata dereva,kumuandikia makosa na kulipa faini na pia kumpoga picha na kuzisambaza mitandaoni ili wahusika waone "uchungu" wa kosa na wengine wajifunze kupitia adhabu hizo

Hii imekuwapo hata kabla ya Rais JPM kutoa pendekezo la askari wa usalama barabarani kukamata magari yanayovunja sheria ya njia za mwendo kasi,kuyapeleka polisi na kufungua magurudumu.

Kikubwa kilichojitokeza ni kuwa wengi wa wavunjaji wa sheria hizo ni "wasomi" na watumishi wa mashirika ya umma na binafsi ambao ilitegemewa ndio wenye uelewa mkubwa na hivyo kuheshimu sheria za barabarani

Hawa ni Baadhi waliokubwa na Adhabu hiyo:Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR