• Breaking News

  Jun 9, 2016

  Sala zetu tuzielekeze kwa Ndungai arejee haraka kuliokoa Jahazi

  Katika Bunge la Katiba, wajumbe UKAWA walimshangaa Dr. Mwakiembe kwa msimamo wake wa kutaka serikali mbili, ilhali katika "thesis" yake ya kupata udaktari alioifanya kuhusu muundo wa muungano wa Tanzania alionyesha sura nyengine ya serikali tatu

  Katika " thesis" yako hiyo alinukuliwa kuwa Serikali tatu ndio muundo unaofaa. Lakini alipokuja kujitetea, alikanusha na kusema "wajumbe wamechukua kipande kimoja tu, wakati walipaswa kusoma sehemu iliobakia" Hoja yake ilionekana kuwa ni ya msingi.

  Jioni hii,Mhe. Tulia akisoma hukumu ya wajumbe wa UKAWA, alinukuu adhabu waliopewa CUF kwa kususia Bunge katika mwaka 1998. Kwa vile Spika anaweza kuchukua hukumu iliowahi kutolewa na Spika waliopita kwa kosa "liliofanana", na hivyo kuwatia hatiani

  Bila ya kufafanua kosa waliofanya CUF la kususia bunge linashabihiana vipi na hili la kumsusia yeye Dr. Tulia (sio bunge).

  Naibu spika ni mwanasheria kitaaluma, anajua kuwa haiwezekani ikiwa yeye ndie anatuhumiwa kuwa chanzo cha mgogoro akawa yeye ndio mwendesha mashtaka na vilivile kuwa Jaji!

  Kama Dr. Tulia anaiishi sheria na kuiheshimu angeweza kukaa pembeni kwa muda kuachia sheria za bunge lichukue hatua stahiki chini ya wenyeviti, halafu angerejea.

  Katika muhimili mwengine wa nchi, yaani mahakama, mtuhumiwa anahaki ya kumkataa Jaji katika shauri lake kama ataona kuwa hatotendewa haki. Seuze huku bungeni kuwa huyo Jaji ndio mtuhumiwa mkuu na ndio chanzo cha tatizo.

  Tusimame kwa pamoja na kusali, kumuombea ndugu Ndungai apone haraka kuja kuliokoa jahazi linalotota kwa mwendo wa kasi. Ama kweli uzuri wa mtu huujui mpaka pale atapokuwa hayupo. Tumuuombee dua njema Ameen

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku