• Breaking News

  Jun 19, 2016

  Tanzania Inawahitaji Watu Aina ya Mch. Gwajima Walau Kumi Hivi....

  Spin Doctoring ni taaluma ya juu sana katika Ujasusi na ili mtu ujifunze ni lazima uwe na kipaji cha hali ya juu cha maswala hayo, ambacho kimsingi mtu huzaliwa nacho.

  Nchini Marekani kuna mtu anaitwa Bob Bekwen, huyu ni jasusi wa CIA, hutumiwa kwenye maswala mengi ya ku spin mambo mengi ndani na nje ya USA hasa kubadili hali ya upepo wa kisiasa,

  Nchini Urusi kuna mtu pia anaitwa Lavrov kwa sasa ni waziri wa Mashauri ya nje, huyu ni jasusi wa shirika la ujasusi la FSB, huyu anatumika zaidi kwenye mashauri ya kidiplomasia

  Uingereza ina mtu anaitwa Tony Blair, huyu amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, lakini kwa sasa anatumika kama special spinning doctor ndani ya shirika la Ujasusi la nchi hiyo la M16, na vilevile anatumika kwenye misheni iitwayo "IC" ya nchi hiyo ndani ya G8, katika hilo ameweza kusaidia taifa hilo kwa kiwango kikubwa.

  Tanzania pia imekuwa na spinning Doctor wazuri wengi japo sio "majasusi", mathalani Dr Slaa, Tundu Lissu, Zitto Kabwe, John Mnyika, Godbless Lema, Salumu Mwalimu nk. Pia yupo bingwa wa wote Tanzania, huyo sio mwingine ni Abdulahman Kinana, huyu ni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania, ametumia kwa ufanisi mkubwa kipawa chake katika siasa za kijana kwa nyakati zote ndani ya chama hicho, lakini kipawa chake hakikuwahi kuwa na mafaa kwa nchi ya Tanzania zaidi ya angamizo tu.

  Ingizo jipya katika medani hizi ni Mchungaji Gwajima huyu ni mmoja ya watu wachache duniani ambao ni special Spinning Doctors ambao taifa limebahatika kuwa nao..... Haimaanishi yeye ni jasusi, lakini tendo alilolitenda lina sura na haiba ya kijasusi.

  Kwa uwezo wake wa ku spin mambo, Gwajima ameweza kubadili upepo wa kisiasa ndani ya ccm, na sasa wamebaki kuhaha kumzima, lakini kundi lililonufaika na spinning hizo ambalo kimsingi ndio la wafanya maamuzi ndani ya chama wala halina presha, yaani limeshinda na 23/07/2016 litafunga kitabu cha nyakati za siasa za ubwa.

  By Yericko Nyerere

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku