Jun 5, 2016

Zitto awaumiza CHADEMA/UKAWA kwa "Linda Demokrasia"

Huu mchezo hauhitaji hasira wala haraka. Kitendo cha chama kikongwe cha upinzani kukopi na kupaste ubunifu wa chama kichanga ( mtoto wake) kwenye harakati zake za linda demokrasia ni udhaifu mkubwa sana.

Najiuliza ACT imewaandikia barua kushirikiana katika suala hilo kuwafikia wananchi lakini hadi hivi leo ACT inazindua operation yake pale Dar UKAWA hawajajibu barua na badala yake wameanzisha ya kwao itakayoanza tarehe 7 juni.

1: Je mlisubiri hadi ACT wabuni operation na nyie mkop? hii ni dalili ya kuishiwa pumzi
2: Je kwanini msipande jukwaa moja na Zitto? mnaogopa nini kwa zitto?
3: Je kwanini msiunde nae hizo team au mngetuma wawakilishi kwenye mikutano ya Zitto ili tujue mu wamoja? Hii ni vita mnayoanza wenyewe lakini sioni kama mtashinda dhidi ya muha huyu.

Mtizamo wangu:
Population ya mkutano wa Zitto pekee itakuwa ni sawa na popolation ya mbowe+lowasa+sumaye. hivyo itadhihirisha Zitto mshindi.
Mnampa kiki Zitto wenyewe bila kujua na mnajichimbia kaburi.Kama fitina mlishindwa mwaka jana saizi zitto anaizika rasmi CHADEMA.
mtatuletea picha na video zenu lakini tukicompare na zitto.CHADEMA chaliii
Zitto wazike hao mana hakuna namna.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR