• Breaking News

  Jun 3, 2016

  Zitto: Simjadili Dr Tulia ni kibaraka, Mdee: Serikali ya Magufuli ni ya kisanii tu!

  Wakihojiwa na redio moja mkoani Kagera inakosemekana wataanzia ziara hivi karibuni Zitto amesema hawezi kumjadili naibu spika maana anajua anatumwa. "Huyu simjadili maana najua anatumwa na akiambiwa geuka anageuka, akiambiwa kimbia anakimbia". Alisema yeye anamwambia aliyemtuma apambane na ufisadi na si demokrasia kwani dunia nzima waliogombana na demokrasia wameangukia pua. Amesisitiza ziara inayotarajia kuanza itawazindua watanzania

  Mdee: Amesema kiini cha kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kutaka kuwaaminisha kwamba serikali hii ni tukufu kumbe ya kisanii tu. Amewataka watanzania wajitokeze kwa maelfu kwenye mikutano yao ili wadadavuliwe serikali ilivyo ya kidikiteta. "Ndani ya bunge tumeaacha wabunge makini wa kuweza kuibana serikali, nje tuko mashine za kutosha kuiamsha jamii ya watanzania".

  Wote wamesema serikali ya Magufuli ina dalili zote za kidikteta na inaliteka bunge makusudi ili kunyamazisha wakosaoji maana huko ndiko Magufuli anaweza kuanikwa. Wamesema madikteta wote hupenda kusifiwa na kuimbiwa nyimbo za kuabudiwa. Walisema

  2 comments:

  1. NA WEWE UNATUMWA NA NANI POLE SANA ZITO TULIZANI MTU KUMBE KILAZA

   ReplyDelete
  2. Watanzania Msipoamka na kufikiri, kutafakari, kupigania uhuru wenu, kuuondoa ukandamizi, kufuga mafisadi wakuu ambao wameapa hawatatumbuliwa kamwe. Wao ni vigogo ambao wamedanganya toto tu. Kiukweli ni kwamba. Mpaka chanzo kikuu cha cha ufisadi kitumbuliwe, au la kila kile kidogo Magufuli alikipapasa hakina maana. Ardhi ya Wamassai kwa kupitia Maendeleo, mazingira, wamepewa Wazungu ambao kwa manipulation wanasema Tanzania maskini, Wamasai Maskini, lakini wamejiingiza kupitia viongozi wakuu wa nchi hii kuwanyan'ganya Wamasai kama nusu watu. Kama huu si wizi ni nini.Wamasai wamezaliwa Umasaini, wamekaa na wanyama pori kwa miaka yote hii pande kwa pande. Mpaka walipofika Wachina, Wazungu, Waarabu kupitia utawala chini ya CCM wamewanyan'ganya Wamasai maeneo yote ambayo ni vigezo vikuu vya uchumi nchini na kuwakabidhi wazungu, Waarabu, Wachina, na kuleta vifo kwa wanachi kupitia enviromental projects zilizoanzishwa na nchi kuu nane duniani na na kupitia globalization ambako Watanzania, Waafrika hawapo kuchangia huu uhujumu wa njia zote kuu za kiuchumi.Wamasai hawakujua ni nini kinaendelea huko. Wengine walipewa vigari, vijishule, vihospitali na kuchukua maeneo yenye thamani ya matrilion yao.
   Leo mnawawanyima Watanzania wote kufuatilia namna gani Tanzania imeingiliwa bila Watanzania kuhusishwa, kuelewa kinachotendeka mbele yao.Je, Watanzania, au mtanzania yeyote anaweza ruhusiwa kufanya hivi kwenye nchi zao? na kama sio je Kwa nini Waafrika, Watanzania Wauzwe hii karne ya ishirini na moja wakati kuna Wasomi wengi Tanzania. Kwa nini Sheria potofu za Tanzania zinakubalika. Kwa nini viongozi watetezi wanahangaishwa. Nilifikiri CCM itabadilika chini ya Magufuli lakini hakuna kitu. Leo Makanisa yanaanza kujionea Wazi na kupata fursa ya kuzungumza lakini wengi wao wanapewa vijipesa vidogo wanakubali kuwapeleka na kuwauza waumini wao na kuwafunga midomo.What happened?
   Hivi Tanzania ni duni kiakili hivi?
   Vijana wengi hawana mwamko wa kizalendo. Wanababaishwa kama tunavyowaona wasanii wengine wakitumiwa na kijibadili kila kukicha. Tanzania na njia kuu za uchumi karibu aslimia 80 zimeuzwa kipindi hiki cha miaka ishirini bila Watanzania kudhihinisha mauzo haya. Sasa wanashangaa imehuwaje. Tulilala chini ya CCM sababu kila mtu alikuwa hai kuchapua chake mapema. Fikirieni mababu zenu, Fikirieni Mzee Nyerere, Mfikirieni Sokoine mtu wa watu.Nyinyi mmeyakuta matunda yameiva wala hamjui thamani yake.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku