• Breaking News

  Jul 26, 2016

  24 waitwa Stars,Msuva,Jeba,Mnyate na Mahundi ndani

  Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini Julai 31 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Nigeria unatarajiwa kuchezwa mwanzoni mwa mwezi Septemba.

  Mkwasa amesema ametoa nafasi kubwa kwa wachezaji vijana ili kuwapa uzoefu na licha ya mechi hiyo kutokuwa na umuhimu wowote kwa timu zote mbili, lakini bado inaumuhimu linapokuja suala la kupanda katika viwango vya FIFA.

  Mkwasa amesema, Kambi itaanza August Mosi mpaka 05 lakini wachezaji watatakiwa kuripoti kambini Julai 31 kwenye kambi ambayo itatajwa hapo baadaye.

  Wachezaji wote wa wanaocheza soka nje ya nchi wataungana na timu moja kwa moja Nigeria na baada ya mchezo huo watarejea tena kwenye vilabu vyao.

  Mkwasa amesema kikosi alichokiita sio cha moja kwa moja hivyo ataangalia pia Ligi itakapoanza iwapo atapata wachezaji wazuri zaidi huku akiwataka makocha wa vilabu kutoa ushirikiano kwa wachezaji walioitwa kujiunga na kambi ya Stars.
  Katika kikosi hicho Mkwasa amewaongeza wachezaji watatu ambao ni Ibrahi Jeba, Joseph Mahundi na Jamal Mnyate huku akiwarudisha Oscar Joshua na Simon Msuva.
  Wachezaji walioitwa kwa ajili ya kambi hiyo ni

  Makipa:
  Deogratius Munish, Beno Kakolanya (Yanga SC), Aishi Manula (Azam FC)
  Walinzi:
  Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Juma Abdul (Yanga SC), Erasto Nyoni, Agrey Morris (Azam FC) Mohamed Hussein (Simba SC).
  Viungo:
  Farid Musa, Himid Mao (Azam FC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto,Jonas Mkude (Simba SC), Ibrahim Rajab ‘Jeba’ (Mtibwa Sugar FC), Hassan Kabunda (Mwadui FC), Simon Msuva, Juma Mahadh (Yanga SC).
  Washambuliaji:
  Joseph Mahundi (Mbeya City), Ibrahim Ajib, Jamal Mnyate (Simba SC), John Bocco (Azam FC) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku