• Breaking News

  Jul 29, 2016

  CHADEMA Yang'ang'ana Kuendelea na Operesheni UKUTA

  Siku chache baada ya Msajili wa vyama vya siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mtungi kukitaka chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kusitisha mpango wao wa kufanya mikutano ya Hadhara pamoja na kongamano hapo Septemba Mosi mwaka huu,hii leo Uongozi wa Chama hicho umeibuka na kudai kuwa mpango wao wa kufanya Operasheni yao waliyooiita UKUTA uko pale pale.
  Akizungumza leo jijini Dar es salaam,Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Bw. Salum Mwalimu amesema Msajili amekua kimya juu ya hali ya siasa na kukandamizwa kwa vyama vya siasa kunakoendelea nchini hivyo hawapo tayari kumsikiluza kutokana naye kuonekana anawakandamiza ili kudidimiza demokrasia nchini.
  Kwa upande Mwingine,Salum Mwalimu akizungumzia kauli aliyotolewa na Msemaji wa chama cha Mapinduzi CCM, Christopher Ole Sendeka kuwa ni bora viongozi wa chama hicho wakaandamana na familia zao na sio kuwashirikisha wananchi,amesema hawapo tayari kumjibu kiongozi huyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku