• Breaking News

  Jul 25, 2016

  Chama cha Democratic cha US chaawaalika Zitto na Maalim Seif

  Wanasiasa, Zitto Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani kwaajili ya kuhudhuria mkutano mkuu wa chama cha Democratic.


  Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

  Wanasiasa hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa cha hicho utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia chama hicho.

  Marekani inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Novemba 8 mwaka huu ambapo Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kuchuana na Donald Trump wa chama cha Republican.

  Akizungumza na gazeti la Mwanahalisi, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo, Abdallah Khamis, amesema, “wakati Zitto akiwa kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa kisiasa duniani.”

  “Kufanya kikao cha maandalizi juu ya ufunguzi wa tawi la wanachama wa ACT Diaspora la nchini Marekani pamoja na kuwa na mazungumzo maalum na Maalim Seif juu ya hali ya kisiasa ya Zanzibar na taifa kwa ujumla,” aliongeza.

  Viongozi hao ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

  BY: EMMY MWAIPOPO

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku