• Breaking News

  Jul 30, 2016

  HATIMAYE Spika wa Bunge, Job Ndugai Arejea Nchini.....

  Spika wa Bunge, Job Ndugai amerejea nchini kutoka India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

  Mbunge huyo wa Kongwa aliondoka nchini Mei kwenda nchini humo, ikiwa ni takribani wiki mbili tangu kuanza kwa Mkutano wa Tatu wa Bunge la Bajeti ambao aliongoza vikao vichache, kipindi cha asubuhi, huku mchana akipokewa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

  Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge, Owen Mwandumbya alisema jana kuwa Ndugai alirejea nchini Julai 27  baada ya  kukaa kwa zaidi ya mwezi mmoja akifanyiwa uchunguzi.

  “Watanzania wasiwe na wasiwasi Spika amerudi na yupo katika afya njema. Maombi yao kwa Ndugai  yalikuwa mengi na Mungu ameyasikia,” alisema Mwandumbya.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku