• Breaking News

  Jul 26, 2016

  Jordan Apinga Ubaguzi wa Rangi Marekani

  Baada ya kipindi cha takribani mwezi, tangu watu weusi kupamba na Polisi nchini, Marekani kwa kile cha kupinga ubaguzi wa rangi, nyota wa zamani wa NBA Michael Jordan, ameahidi kutoa fedha, kuchangia harakati za kukomesha ubaguzi huo.

  Gwiji wa mpira wa kikapu, Michael Jordan ameongea kuhusu ubaguzi wa rangi uliopo nchini Marekani sasa hivi na amesema atachangia dola milioni mbili kwa ajili ya kusaidia mahusiano mazuri.

  Mchezaji huyo wa zamani wa Chicago Bulls, ambaye alikosolewa kwa ukimya wake kuhusu mambo ya kisiasa wakati alipokuwa bado anacheza mpira wa kikapu, hawezi kuendelea kuwa kimya.

  Maneneo ya Jordan, yanakuja baada ya Polisi kuuwa Wamarekani wawili wanaume, wenye asili ya Africa, , Alton Sterling na Philando Castile, kwenye miji ya Dallas na Baton Rouge.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku