Jul 29, 2016

Kisa ‘Unga’, Chris Brown Apoteza Mvuto

STAA wa muziki, Chris Brown amepoteza mvuto wake kisura kisa kikiwa ni madawa ya kulevya ambayo aliwahi kukiri kutumia mwaka mmoja uliopita.

Mtandao mmoja umetupia picha yake inayoonesha jinsi alivyoathirika na dawa na ukaeleza kuwa anatia huruma kwa sasa kwani ngozi yake imepauka sana na macho yake yamepoteza mvuto aliokuwa nao kabla ya kutumia dawa hizo.

Aliyekuwa meneja wake Mike G alisema kuwa Chris Brown amekuwa akitumia dawa na anapokuwa kwenye hali ya ulevi anakuwa mkorofi kupita maelezo.

Mashabiki wake walioona picha hizo walimuonea huruma na wameomba asaidiwe katika kumrudisha kwenye muonekano wake wa zamani wakiamini yeye ni brazameni aliyejiharibu.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR