Mwanamuziki maarufu nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Koffie Olomide, amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela.

Hukumu hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita kusambaa kwa video inayomuonesha akimpiga teke dancer wake wakati wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JKIA jijini Nairobi alikokuwa atumbuize Jumamosi iliyopita.

Kufuatia tukio hilo alifukuzwa nchini humo na show yake kusitishwa. Show nyingine aliyokuwa aifanya nchini Zambia ilisitishwa siku chache baadaye.

Kwa mujibu wa mtandao wa Voice of Congo, hukumu hiyo imependekezwa na mwanasheria mkuu wa serikali. Staa huyo alikamatwa nyumbani kwake wiki hii.

Japokuwa bado hakujatoka taarifa ya kina, imedaiwa kuwa hukumu hiyo haina faini ikimaanisha kuwa Olomide lazima aende jela.


Post a Comment

 
Top