Jul 31, 2016

Lembeli Aibuka Mkutano wa Rais Magufuli

Mbunge wa zamani wa jimbo la Kahama, James Lembeli aliyehamia Chadema ameibuka leo katika mkutano wa na Rais John Magufuli uliofanyika mjini Kahama.

Akihutubia wananchi wa Kahama, Rais Magufuli amemkaribisha Lembeli na kumtaka kurudi  CCM akisema kwa Tanzania anayoijua yeye hatakuwa amepoteza mkia, kwani huko aliko ndiko mafisadi wamekimbilia.

Hivi karibuni akihutubia mkutano Mkuu wa CCM, Rais Magufuli akizungumzia waliotoka kwenye chama na kurejea tena, alitoa mfano wa ng’ombe aliyekatwa mkia, akisema huwezi kumzuia kurejea zizini lakini wenzake wanamkua kuwa hana mkia.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lembeli amesema amekwenda kwenye mkutano huo kwa kuwa kazi anayoifanya Rais Magufuli ndiyo ambayo alikuwa anapigania wakati akiwa

mbunge kwa kuwa Shinyanga rushwa ilikuwa imekithiri.

Amesema na  hawezi kurudi CCM mpaka Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho akisafishe.

"Kubadilisha msikiti siyo kuacha Uislamu, nyumba itaposafishika nitarudi," amesema Lembeli.
Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR