Jul 30, 2016

Licha ya Rais Kupiga Mkwala..Chadema Wasisitiza Maandamano yapo Pale Pale


Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuendelea na dhamira yake ya kufanya maandamano nchi nzima ifikapo  Septemba Mosi, mwaka huu licha ya Rais John Magufuli kutoa tahadhari dhidi ya kitendo hicho leo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Singida.

Hayo yamesemwa usiku huu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel Ten jijini Dar es Salaam.

“Lengo letu tunataka kuwaeleza wananchi hasa wanachama wa chama chetu maazimio tuliyokubaliana katika mkutano wetu uliomalizika hivi karibuni,” amesema Dk Mashinji.

Amesema Chadema hawakusudii kufanya vurugu bali watafanya maandamano ya amani yanayolenga kwenda kupokea taarifa ya mkutano.

“Nashangaa ni kwanini maandamano haya yanawatia hofu watawala kiasi cha kutaka kuyazuia na wala hatuhitaji ulinzi wa polisi, tutaenda kwa amani tu,” amesema katibu mkuu huyo.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR