Jul 31, 2016

Lowassa, Nape na Mbowe Wakutana Uso Kwa Uso Msibani

Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema na Ukawa, Edward Lowassa amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Mnauye leo katika jumuiko la kuuaga mwili wa aliyekuwa Mpigapicha wa Tanzania Daima, Joseph Senga.

Mwili wa Joseph Senga (58) umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwao, Shushi-Nyambichi, Kwimba mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko hapo kesho.

Akizungumza wakati wa kuuga mwili wa marehemu Dar es Salaam mapema leo, msemaji wa familia, Charles Kapama amesema maziko yatafanyika kesho saa nane mchana baada ya mwili kuwasili kijijini.

Viongozi mbalimbali walijumuika na ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo kuuga mwili wa marehemu Senga ambaye alifariki dunia Julai 27 katika hispitali ya BLK, New Dehli India alikokwenda kupatiwa matibabu, katika uwanja wa mpira uliojirani na nyumbani kwake, Sinza jijini hapa.

Viongozi hao ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.

Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA

Post a Comment

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © Siasa Huru l Habari za Siasa | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by SiasaHuru.com