• Breaking News

  Jul 26, 2016

  Lowassa ndiye Aliibakiza CCM Madarakani

  Bavicha hebu kumbukeni vizuri juu ya raisi wenu mliyemwandaa kwa muda wa miaka minne, kuzunguka nchi nzima kwa usafiri wa Chopa sijui mliziazima wapi maana nimezimiss kweli kweli, wataka mabadiliko ya kweli wakawaunga mkono, ila kwa masaa machache tu mzee wa amri akabadili gia angani, akabadili na vichwa vyenu, mambo yakageka.

  Akaja mliyekuwa mnampinga kwa nguvu zenu zote kwa miaka minne, akawapima akajua mna njaa, akawapa kauli mbiu ya safari ya matumaini, akajua elimu hamna, akawapa matumaini ya ELIMU, ELIMU, ELIMU kwa kuiweka elimu ya mtoto wa miaka mitatu hadi wa miaka hamsini, yaani chekechea hadi chuo kikuu kwenye chungu kimoja japo elimu hiyo imegawanyika katika elimu ya awali, hadi elimu ya juu ila yeye kachanganya sehemu moja yote! Yaani ni sawa na uwaweke wanafunzi wote kuanzia chekechea hadi chuo kikuu darasa moja halafu uwafundishe wimbo: ELIMU, ELIMU, ELIMU na wote wanaitikia!

  Maji ukiyapiga kwa fimbo au kitu chochote, hayatawanyiki kuelekea upande mmoja, bali pande zote. Hivyo ujio wa Lowasa Chadema uliwatawanya wanachama wake, wapenzi na mashabiki. Katika mtawanyo huo, wapo waliorudi na kuenda naye kwenye kuzungusha mikono a.k.a safari ya mabadiliko, pia wapo ambao baada ya kutawanywa hawakurudi hadi wa leo.

  Mtawanyo huo ndiyo mwanzo wa kushindwa kwa upinzani na CCM kuendelea kubaki madarakani. Ndiyo maana Simba katika mawindo yake, kama anakimbiza swala, halafu akakutana na nguruwe, ataendelea kumkimbiza swala hatahangaika na nguruwe. Hii ina maana mahali Bavicha walipotea ni hapa kuacha kukimbiza swala waliyekwishaanza kumkimbiza na kukimbiza nguruwe na mwishowe wakakosa wote na hii inadhihirisha wanyama kama simba wana akili kuliko Bavicha huku Mwenyezi Mungu ametupa utashi wa kutawala wanyama hao.

  Bavicha kama hamuamini lengo la Lowasa ni kuendelea kuibakiza CCM madarakani miaka 50 ijayo kama alivyowatamkia, basi endeleeni na safari ya kuelekea 2020 na Lowasa muone tena kichapo toka CCM. Kwa leo ni hayo tu, nawatakia tafakari njema

  Maoni Huru Kutoka Kwa Sirluta/JF

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku