• Breaking News

  Jul 25, 2016

  Madrid Walimtosa Pogba Mara Mbili

  MADRID, HISPANIA. PAUL Pogba wakati wowote wiki hii huenda akatua Man United kwa pesa ya maana, lakini imefichuka kuwa Rais wa Real Madrid, Florentino Perez alimkataa mara mbili katika klabu yake.

  Baada ya kuona hali kuwa hivyo licha ya kocha wa Real, Zinedine Zidane kukiri anamkubali kiungo huyo, Pogba sasa mawazo yake ni kurejea Old Trafford.

  Ripoti zimefichua kwamba Pogba mara mbili tofauti alipelekewa ofa Real Madrid, lakini Perez alimkataa.

  Kwanza ilikuwa mwaka 2012 mkataba wake ulipofika mwisho Man United lakini Perez alijipa imani kwamba kwa kuwa United walimuachia kirahisi basi hawezi kuwa bora.

  Mara ya pili ilikuwa mwaka 2014, meneja mkuu wa Real, Jose Angel Sanchez alizungumza na Juventus na kukubaliana ada ya Euro 60 milioni lakini Perez tena akamkataa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku