• Breaking News

  Jul 30, 2016

  Magufuli: Wapinzani Walisusia Vikao Vya Bunge Kwa Sababu Wanajua na Wao ni Part ya Mafisadi.....Naahidi Ntawanyoosha!!!!

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana  July 29 2016 alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo alizungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

  Akizungumza na wananchi wa Manyoni mkoani Singida Rais Magufuli alizungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge  kwa kujiziba  midomo na makaratasi

  Alisema wabunge hao wa upinzani waliamua kususia  bunge kwa sababu kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya bunge ni mahakama ya mafisadi na wao (wapinzani)  ni sehemu ya mafisadi .

  "Hawakuingia kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke" Alisema Rais Magufuli

  Msikilize Hapa:

  1 comment:

  1. Na maraisi waliouachia Ufisadi ungurume Je ni lini utawatumbua. Hawa ndio chanzo. Walikuwaje watawala kwa miaka hii yote. Ukiwatumbua hawa kwanza nadhani kazi itakayobaki ni nyepesi sana. Lakini huwezi kuondo kijiti ukaacha banzi kuu. Ni lazima wote wafyekwe. Kama katiba ya zamani hairuhusu, katiba hiyohiyo inasema Sheria za nchi zifuatwe. Hapa kuna utata mkubwa sana ndo maana Wasomi wanaozichambua sheria zetu ingawa wanakukubalia utumbue kakini sheria zimevunjwa inabidi zote ziwe sawa bila ubanguzi wa cheo cha mtu, jinsia, rangi wala kabila. Hapa kuna makosa.Tumbua wote mpaka maraisi walisababisha wewe uje utumbue. Hapa utakuwa shujaa wa kwanza nchini na wengi watakusapoti.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku