Jul 14, 2016

Mahakama yatupilia mbali mapingamizi kesi inayomkabili Tundu Lisu

Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam imetupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na wakili wa utetezi wa kesi inayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lisu pamoja na wenzake watatu  katika mashtaka ya kuandika habari ya uchochezi kwenye gazeti la MAWIO ambalo limefutwa na serikali.

Yaondoa mashtaka mawili kati ya matano  yanayomkabili Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA Tundu Lisu pamoja na wenzake watatu  katika mashtaka ya kuandika habari ya uchochezi kwenye gazeti la MAWIO ambalo limefutwa na serikali.

Inadaiwa washtakiwa hao , Tundu Lissu , Simon Mkina , Ismail Menboob na Yusuph Abood, Januari 12 hadi 14, 2016 katika jiji la Dar es Salaam, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa  za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, Ă«Machafuko yaja ZanzibarĂ­.

Mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Wakili wa upande wa Jamhuri, Paul Kadushi,amemsomea Lisu Mashtaka  ya uchochezi yanayomkabili baada ya awali kutokutokea mahakamani hapo wakati kesi ilipokuja kwa mara ya kwanza.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili PETER KIBATALA  uliibua hoja za kisheria na kuitaka mahakama kufuta mashtaka mawili  kwa madai kwamba yalikuwa hayaja ambatana na kibali cha mwanasheria mkuu wa serikali  ambalo ni hitaji la kisheria , na kwakuwa vurugu hizo zingetokea zbar hivyo , mahakama ya kisutu haina mamlaka wa kusikiliza mashtaka hayo  na pia maelezo ya kesi hayajitoshelezi.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR