Makazi mapya ya waziri mkuu wa Uingereza aliyejiuzulu bwana David David Cameron yana thamani ya Euro milioni 17 yakiwa mtaa wa Holland Park.

David Cameron ameondoka kwenye makazi yake kikazi yaliyoko Downing Street yeye na familia yake alikokaa kwa muda wa miaka sita, akitumikia nafasi ya waziri mkuu kabla ya kujiuzulu. Makazi yake mapya yenye vyumba saba vya kulala yapo upande wa magharibi mwa Jiji la London.

David na mkewe Samantha Cameron na watoto wao watatu waliondoka kwenye makazi hayo jana mchana na kusindikizwa na kikosi maalum cha polisi hadi Holland Park.

Kiongozi huyo wa zamani wa Uingereza ataishi hapo mpaka tamati ya kodi kwenye nyumba yake yenye thamani ya Euro milioni 3.6 ambayo ameipangisha.

Pia ataishi hapo ili kuwa jirani na shule ambayo watoto wake watatu Nancy 12, Elwen 10, na Florence 5, wanasoma.


Post a Comment

 
Top