Jul 30, 2016

Mbunge Professor J Kufunga Ndoa na Mama Watoto Wake

Mchawi wa Rhymes na mbunge wa Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amesema hivi karibuni atafunga ndoa na Mama watoto wake ‘Mama Lisa’ ambaye tayari ameshadumu naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Rapper huyo ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Kazi Kazi’ akiwa ameshirikisha Sholo Mwamba, amekiambia kipindi cha FNL cha East Africa Television Ijumaa hii kuwa yupo kwenye maandalizi ya kufunga ndoa.

“Very soon naingia kwenye maisha ndoa,” alisema Professor. “Wakati naingia kwenye majukumu mapya haya hata mke wangu aliniruhusu hebu tumikia wananchi alafu baadae kila kitu kitakuwa sawa, very soon, very soon jiandaeni na kadi zangu,”

Pia rapper huyo amesema yeye haamini kama kuoa kunaweza kumsababishia msanii wa muziki kushuka na kupoteza baadhi ya mashabiki.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR