Jul 31, 2016

Mkurugenzi Bagamoyo atumbuliwa baada ya siku 24


Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi ( aliyesimama) ametumbuliwa na Rais John Magufuli baada ya kufanya kazi kwa siku 24 tangu ateuliwe.

Azimina ambaye aliteuliwa Julai 7 mwaka huu uteuzi wake umetenguliwa na Dk Magufuli  kwa kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Kutenguliwa huko kulifanyika jana kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais(Tamisemi), Musa  Iyombe.

No comments:

Post a Comment