• Breaking News

  Jul 31, 2016

  Mtuhumiwa wa Mauaji Mwanza Auawa Mikononi Mwa Polisi...

  Mtuhumiwa wa ujambazi Msafiri Suleiman maarufu kama Juma Msukuma ameuawa wakati akijaribu kutoroka mikononi mwa polisi waliokuwa wameshikiria Julai 28 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni katika  eneo la Igoma kata ya Igoma jijini Mwanza.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema mtuhumiwa siku hiyo alikuwa amekamatwa na Polisi akituhumiwa kufanya matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha akishirikiana na wenzake watatu na kuwataja wenzake kuwa ni Jackson Magesa ( Nyakibimbi), Samwel Mwita na Boniphace Nyamhanga. Kamanda alisema baada ya mahojiano na polisi mtuhumiwa alikiri kuhusika na uhalifu na akakubali kwenda kuwaonesha askari sehemu aliyoficha silaha maeneo ya Buhongwa mlimani.

  Alisema walipofika eneo husika aliwaonesha mkasi mkubwa wa kukatia vyuma na kipande cha nondo, huku akiwathibitishia kuwa silaha alikuwa ameichimbia ardhini katika eneo hilo.

  “Wakati askari wakiwa kwenye harakati za kufukua ili waichukue silaha hiyo, mtuhumiwa alitumia mwanya huo kuanza kukimbia huku akiwa na pingu mkononi, askari walifyatua hewani risasi tatu, lakini mtuhumiwa hakutii amri hiyo ndipo alipopigwa risasi mguuni na kufanikiwa kukamatwa”,

  Aidha mtuhumiwa huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitali.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku