• Breaking News

  Jul 29, 2016

  Mwanamuziki Malaika Afuatwa na Freemason

  Mwanadada mkali wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wa “nawararua” Malaika ajikuta kwenye mtego wa kuwindwa na Freemason.


  Hivi karibuni Malaika amekuwa mmoja kati ya wasanii wanaosadikiwa kujiunga na dini ya Freemason, na akituhumiwa kwamba baadhi ya mambo yanayomzunguka ni ishara au alama za freemason ikiwemo jina lake la Iluminati, mapozi ya picha zake pamoja na namba yake ya simu kuwa na sita sita (666) mwishoni.

  Malaika akiongea na eNewz alisema kwamba “kwa kweli nashindwa kupata jibu sahihi lakini ni kweli nilishafuatwa na watu ambao wapo katika hiyo Freemason, hata hivyo siwezi kulizungumzia zaidi ya hapo, Pia namba yangu ya simu ina 666 na namba sita kwangu inamaana nyingi saana na imebeba maisha yangu pia ”.

  “Mwache mtu akuhukumu kutokana na vile anavyotakiwa akuhukumu na once ukitoka tumboni kwa mama yako watu walikuongelea na mpaka unaanza maisha yako wanakuongelea so waache watu wakuzungumzie inakuwa ni vizuri zaidi” aliendelea kusisitiza Malaika.

  Alimalizia kwa kusema “Mimi ni mcheshi saana lakini pia mashabiki zangu wategemee kazi nzuri. Yataibuka mambo mengi ya 'ufreemason' lakini tunajaribu tu kutengeneza mziki mzuri na kwa kipindi hiki nimefanya kazi na watu wa nje ya Tanzania.

  1 comment:

  1. Upumabvu tu sasa si unyooshe maelezo kama ni kweli au si kweli...mengine pumba za kipuuzi kabisa...no wonder huna mashabiki...eti namba sita imebeba maisha yako...kwa hiyo pumzi yako ni namba sita...acha kukufuru wewe jitu zima sifuri..mixxeeww...tupeleke watoto shule jamn itawasaidia hata kujieleza...wakiwa wanahojiwa...

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku