• Breaking News

  Jul 26, 2016

  Nani Kamfukuza Rais wetu Dar??

  Mh Rais na Serikali yake hawakuwa na mpango wa kuhamia Dodoma at least mpaka may mwaka huu na sijui hii ghafla kashauliwa na nani. Hebu angalia yafuatayo


  • Kama angekuwa na huu mpango katika bujeti ya 2016/2017 wangeweka fungu la kuhama, lakini hakuna fungu la serikali kuhama katika bajeti hii
  • Kama angepanga kuhama mapema kiasi hiki waziri mkuu katika majumuisho yake katika bunge la bajeti angetoa taarifa hii ili kuwapa mawaziri taarifa rasmi na muda wa kuhama. lakini hili halikufanyika
  • Kama angekuwa na mpango wa kuhama, nna uhakika asingepeleka bil 12 mahakamani kwa mkupuo wakati wizara zake zote hazina bujeti ya kuhamia Dodoma katika fedha walizotenga.
  • Kama angekuwa na mpango wa kuhama mapema kiasi hiki asingejikita katika ujenzi wa flyover Dar eti ili kupunguza foleni wakati barabara za Dodoma ni nyembamba ka mti, angesubili serikali ihamie Dodoma ili wafanye assessment kama bado kuna ulazima wa hizo flyover Dar hasa baada ya wafanyakazi wa serikali kuhamia Dodoma
  • Kama angekuwa anampango wa kuhama mapema, asingezuia miradi mipya ya NHC kuendelea hasa ile ya Dodoma, kwa kuzingatia uhitaji wa nyumba utakaoongezeka katika mji huo mkuu

  Kwa sababu hizi na nyingine lukuki, napatwa na wasiwasi, nani kamfukuza Mh Rais Dar? Magogoni kuna nini?

  By Songoka/ Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku