• Breaking News

  Jul 24, 2016

  Pamoja ya Yote Lakini Kuna Kubwa la Kujifunza Toka CCM

  Kwanza niseme tu kuwa mimi naunga mkono upinzani, lakini nimeona kuandika uzi huu baada ya kuona kuna kitu ambacho sisi wapinzani tunachakujifunza toka kwa CCM. Pamoja na mapungufu mengi ya chama tawala lakini bado angalau wana mifumo ya kidemocrasia hata kama haijakamilika lakini kitendo cha kubadirisha viongozi wakuu kwenye chama ni kitu cha kuigwa. Hivi ndani ya vyama vyetu hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza?? Kwamba lazima wawe ni wale wale tu. Lini Mbowe atapumzika, Lini Maalim Seif atapumzika, lini Mbatia atapumzika du, na isingekuwa mvutano pengine na Lipumba angekuwemo mpaka leo. Tunahitaji fikra mpya ndani ya vyama vya upinzani kama ni kweli tunahubiri democrasia. Inawezekana nikawa kinyume na wengi lakini, nimeona niwe muwazi kutoa maoni yangu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku