Jul 14, 2016

Rais Magufuli Alishukia Jeshi la Kujenga Taifa JKT Kwa Kushindwa Kukamilisha Kwa Wakati Utengenezaji wa Madawati


Rais John Magufuli amelishukia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza kwa kushindwa kukamilisha kwa wakati utengenezaji wa madawati 120,000 wakati yana askari na idadi kubwa ya wafungwa wanaoweza kuifanya kazi hiyo kwa muda mfupi.

Huku akisisitiza kuwa utengenezaji wa madawati ni operesheni maalumu, Dk Magufuli ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitishia kutoidhinisha fedha nyingine kwa majeshi hayo kwa ajili ya kukamilisha utengenezaji wa awamu ya pili ya madawati 60,000.

Kiasi cha Sh6 bilioni kilichotumika kutengeneza madawati yote 120,000 kimetokana na Bunge kubana matumizi na kurejesha serikalini fedha zilizokuwa hazina umuhimu na kumkabidhi Rais, Aprili 11 kwa ajili ya kutengeneza madawati nchi nzima. Wakati akipokea hundi ya fedha hizo, Rais Magufuli aliagiza Magereza na JKT kutengeneza madawati 120,000 huku kila moja likigharimu Sh50,000.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR