• Breaking News

  Jul 28, 2016

  Rais Magufuli Atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Dkt. James Munanka Wanyancha.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) Dkt. James Munanka Wanyancha.
  Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa leo Mjini Dodoma imeeleza kuwa Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kuanzia leo tarehe 28 Julai, 2016.
  Kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Joseph Odo Haule kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mfuko wa Barabara.
  Uteuzi wa Bw. Joseph Odo Haule umeanza leo tarehe 28 Julai, 2016.
  Kabla ya uteuzi huo Bw. Joseph Odo Haule alikuwa Meneja wa Mfuko wa Barabara (Road Fund).
  Wajumbe wengine wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wanaendelea katika nafasi zao.
  Gerson MsigwaKaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULUDodoma
  28 Julai, 2016

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku