• Breaking News

  Jul 30, 2016

  Serikali ifanye haya kutokomeza mimba za utotoni. Kuwafunga watu miaka 30 siyo suluhisho

  'KUWAFUNGA; NI KUTUACHIA YATIMA PASIPO ULAZIMA SISI, WAZAZI NA WAJUKUU ZETU NDIO TUTAKAOUMIA NA HILO.''

  Kuna mswada ule uliopelekwa bungeni kuhusu wale wanaowatia mimba watoto waliochini ya miaka 18, Napongeza kwa hatua hiyo ya dhati ya serikali kuthubutu kuonesha nia ina mpango wa kupunguza mimba za utotoni; Mswada huo ukipita na kuwa sheria bado hauta tatua moja kwa moja hili tatizo la mimba za utotoni kutokana na kwamba halitakuwa suruhisho bali Tutakuwa tunatengeneza matatizo mengine ambayo ni makubwa zaidi kuliko hata tatizo lenyewe kama ifuatavyo;

  1. Hii sheria endapo mtuhumiwa atafungwa miaka 30, itasababisha ongezeko la watoto tegemezi mtaani kwakuwa majukumu ya kulea huyo mtoto yatafanywa na watu wengine.

  2. Itasababisha sisi wazazi wa mabinti waliotiwa mimba tuhakikishe tunayamaliza kifamilia na wakwe zetu (watia mimba wa wanetu) kwa kuhofia kuachiwa mzigo huo mkubwa wa kulea wajukuu kwa miaka 30 bila msaada na kuongeza makali ya maisha.

  3. Tunawanyima haki wajukuu zetu watakaozaliwa kuwaona baba zao kwa miaka 30 kwa kuishi kama yatima jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu.

  4. Watoto hawa wanaweza kuwa wapo kwenye hatari kubwa ya kukosa maadili katika maisha yao yote.

  5. Itachangia sana sana kwa kupunguza upendo baadhi ya wazazi kuwachukia hasa wapatapo/wazaapo watoto wa kike na kuongeza mfumo dume hapa nchini kwa kuwanyanyapaa.

  6. Hao mabinti watawaficha mabwana zao kwa kuhofia kukosa misaada endapo wakifungwa jera.

  7. Kwa sheria hiyo; serikali itakuwa imeongeza kwa kasi kubwa utoaji wa mimba kwa mabinti zetu kwani watalazimika kuzitoa kwa gharama yeyote ile pasipo hata kujali athari ya afya kimwili na kiimani kitu ambacho kitachangia vifo kwa mabinti zetu kupitia huu utoaji mimba.

  8. Hii sheria itahitaji uthibitisho wa madaktali (DNA) kuhusu ukweli wa jambo lenyewe kwa mtuhumiwa iwapo ni kweli kahusika kumpa ujauzito au la! Ili kuepusha visasi na kubambikiana kesi hizi kimajungu.

  9. Kwa uthibitisho huo wa madaktali; serikali itawajibika kutafta ukweli kwakuwa na madaktali wa kutosha nchi nzima hadi vijijini vinginevyo sheria hii itafanya kazi mjini tu.

  10. Tutapoteza nguvu kazi ya vijana wetu wengi kwa kuwafunga miaka 30 jela; wakati kuna njia mbadala wa kumaliza jambo hilo Kwakuwa lengo nikutokomeza na si kukomoana.

  Note; Sheria hiyo ya miaka 30 jera itumike kwa matukio maalum ya kikatili ya ubakaji bila kujali kabakwa nani, awe mtoto wa shule au mama mtu mzima ie. Kama tukio la kule morogoro n,k.. LAKINI KWA WATOTO WETU WALIOTIWA MIMBA MASHULENI KWA RIDHAA YAO SISI WAZAZI NDIO TUTAKAOUMIA.

  Nashauri haya yafanyike Mbadala ili kutokomeza hizi mimba za utotoni kirahisi kabisa:

  1. Zitolewe semina kwa walimu ili wawafundishe watoto wa kike mashuleni Atthari za kujamiiana chini ya miaka 18; kiafya na kielimu.pia wazazi na jamii nzima Tupige marufuku uvaaji Wa vimini Kwa watoto kuwa endapo mtoto akionekana kavaa akamatwe na kuadhibiwa na wazazi wapigwe faini Kwa malez mabovu.

  2. Masomo ya afya ya uzazi mashuleni (reproduction system) yafundishwe kijinsia(Gender teaching) , Wanafunzi wa kike wasifundishwe wakiwa mchanganyiko na wakiume- Kwani haya masomo yanapofanyika kwa pamoja na wanaume, yanawaongezea sana watoto wa kike ujasiri wa kutokuwaogopa wanaume kihisia, pia hulahisisha sana kutongozana wao kwa wao .

  3. Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii iweke mikakati ya kupima bikira za wanafunzi kila mara na wawe na kadi maalumu kama zilivyo za kliniki za watoto, wapimwe wakiwa darasa la 4,5 na la 7 kwa shule ya msingi. Na kabla ya kujiunga form 1 wapimwe, pia fom 2,3,4,5 na 6 wapimwe kila waanzapo na wamalizapo mhura wa masomo. Kama hilo watashindwa,basi wapime hizo bikira japo mara moja moja darasa la 7, form 2,4,5 na 6 lengo nikuongeza hofu, pia kwa watoto mabikira wapate motisha za kupewa kipaumbele kukaa hostel kuliko wengine n.k

  4. Serikali kupitia wizara ya elimu na ustawi wa jamii; iweke mikakati mathubuti mashuleni kwa kuweka mpango maalumu wa (periodic pregnant testing for student ); kwa darasa la 5 na la 7 kwa shule za msingi, kwa secondary fomu one hadi formu 4 wapimwe hata kila mwaka, hii itaongeza hofu kwa wanafunzi wenyewe na wazazi watashiriki kwa ukamilifu kusimamia zoezi hilo.

  Hayo yote yataenda sambamba na wale wote wanaoonekana kujihusisha na mapenzi shuleni ili wakanywe ama waondolewe kabisa mashuleni kwa Suspension na wale wote wenye kuthibitishwa kuwa na mahusiano na mwanafunzi kimapenzi wakamatwe mara moja; hilo likifanyika litasaidia kutisha wengine kutojihusisha na mapenzi mashuleni…hilo hata sisi wazazi tutashiriki kwa hali na mali kulitekeleza.

  5. Mpango huo wa kuwapima watoto kila mara; utatumika kama tangazo la kupinga mimba za utotoni, kwahiyo utasambaa hadi huko vijinini kupitia kwa wanafunzi wenyewe.

  6. Maadili yatalejea kwa watoto na pengine hata wakafika chuo na bikira zao.

  7. Taifa litapata mama bora na wenye familia na maadili.

  8. Sisi wazazi tutajivunia pia kuzaa watoto wa kike kwa maana tutakuwa naimani wapo katika jamii salama tofauti na presha tulizo nazo sasa.

  KUWAFUNGA WATIA MIMBA NI KUTENGENEZA TATIZO JINGINE KUBWA ZAIDI.

  NAOMBA KUWASILISHA MSWADA HUU, KARIBUNI TUJADILI WADAU.

  NB: Kama una hoja tofauti/mbadala ya kutokomeza mimba iweke hapa pia ijadiliwe.
  Updates;
  Tazama video ya wabunge wanaochangia juu ya hili moja kwa moja hapa

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku